Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:15

Kiongozi wa kijeshi Sudan atetea mkataba na Israel


Generali Abdel Fattah al-Burhan
Generali Abdel Fattah al-Burhan

Serikali ya Sudan inakumbana na hali ngumu ya kiuchumi, ikiwemo mfumuko mkubwa wa bei, sarafu dhaifu na ukosefu wa bidhaa za msingi.

Kiongozi wa serikali ya mpito nchini Sudan, ametetea mkataba wa kurejesha uhusiano kati ya nchi hiyo na Israel ambao ulisimamiwa na Marekani, akisema kwamba mkataba huo haujakamilika lakini utakuwa wa manufaa makubwa kiuchumi kwa Sudan.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa umma kuhusu mkataba huo, Abdel Fattah al-Burhan amesema kwamba alishauriana na waziri mkuu na viongozi wengine wa kisiasa kabla ya mkataba huo kutangazwa Ijumaa wiki iliyopita katika mazungumzo ya sim una rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Hatua hiyo ina utata nchini Sudan, ambayo imekuwa mkosoaji mkubwa wa Isreal na imezua pingamizi kati ya makundi ya kisiasa.

“Napendelea kuuita mkataba huo kuwa wa maridhjiano badala ya kusema ni wa kuleta utulivu,” Burhan amesema katika mahojiano yaliyopeperusha na televisheni ya taifa, akiongezea kwamba “hadi sasa, hatujafikia makubaliano. Tutasaini na wahusika wale wengine wawili, Marekani na Israel, kwa msingi wa ushirikiano.”

Burhan anaongoza baraza lenye viongozi wa kijeshi na kiraia, ambalo lilichukua hatamu za uongozi wa Sudan baada ya kupinduliwa kwa Omar al-Bashir mwaka uliopita, kupitia maandamano.

Serikali ya Sudan inakumbana na hali ngumu ya kiuchumi, ikiwemo mfumuko mkubwa wa bei, sarafu dhaifu na ukosefu wa bidhaa za msingi.

Sudan ilipata afueni wiki iliyopita baada ya Marekani kuthibitisha kwamba itaiondoa Kahrtoum katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi duniani.

Hatua ya Sudan kuwa kwenye orodha ya wafadhili wa ugaidi duniani ilikuwa imeizuia kupata misaada ya kifedha ya kimataifa na kusamehewa madeni.

Wasudan wengi walichukulia hatua hiyo kuwa nzuri na iliyochelewa kupatikana, wakiishurutisha serikali kuharakisha utekelezaji wake kwa kukubali mkataba wa ushirikiano na Israel.

“Hatukulaghaiwa,” amesema Burhan. “Tulieleza maslahi yet una tukapata mambo yanayotufaa, na huenda tutafaidhika sana kuliko wahusika wengine.”

Burhan amesema kwamba uhusiano kati ya jeshi na raia katika baraza la utawala umeimarika sana, na kwamba amefikia makubaliano na viongozi wa kisiasa wanaoakilisha raia kwamba mkataba na Israel unastahili kuidhinisha na bunge, ambalo bado halijaundwa.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG