Wameeleza dozi hiyo huenda ikahitajika baada ya kati ya miezi 9 hadi 12 ya watu kupata dozi mbili za awali.
David Kessler Mwanasayansi Mkuu katika Tume ya Rais Joe Biden ya kukabiliana na janga la COVID-19 amesema wakati utafiti unafanyika huenda chanjo ya kuongeza nguvu ya hizo za awali ikahitajika.
Wakati huo huo afisa mtendaji wa kampuni ya
Albert Bourla anasema huenda watu wakahitaji dozi ya tatu ya chanjo ya COVID-19 katika kipindi cha mieizi 12 kijacho na huenda wakahitaji chanjo za kila mwaka.
Takwimu za awali zinaonyesha kwamba chanjo za kampuni za Moderna na Pfizer na BioNTech zinabaki kuwa na nguvu kwa angalau miezi sita, hata hivyo haifahamiki nguvu zake zinaweza kubaki kwa muda gani kwa ujumla.