Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:19

Biden akutana na wanahabari kufafanua mpango wake wa Covid-19


Rais wa Marekani, Joe Biden
Rais wa Marekani, Joe Biden

Rais wa Marekani, Joe Biden, Alhamisi amekutana na waandishi wa habari kufafanua mpango wa kitaifa wa kugawa chanjo ya covid 19, na kufikia watu millioni 200 nchini kote katika siku 100 za mwanzo za utawala wake.

Mwishoni mwa mwezi Januari, siku chache baada ya kuapishwa, Biden alisema anakusudia kugawa chanjo millioni 150 katika siku 100 za mwanzo za uongozi wake, lakini utawala wake ulipunguza makadirio hayo.

Chanjo millioni 130 zilikua zimekwisha tolewa kufikia jumatano, kwa mujibu wa maafisa wa White House, huku watu millioni 85 wakiwa wamekwisha pata dozi moja, wengine millioni 45 wakiwa wamepewa dozi mbili zinazohitajika.

Kampuni 3 za kutengeneza chanjo, Pfizer-BioNTech, Moderna na Johnson &Johnson ziliahidi kugawa chanjo za kutosha kwa watu wazima millioni 260 hapa marekani ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao, lengo lingine lililotangazwa na Biden.

XS
SM
MD
LG