Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:40

Cameroon yapata chanjo ya Covid-19 kutoka China


Cameroon Jumapili imepokea dozi 200,000 za chanjo ya Covid-19 aina ya Sinopham kutoka China, ambayo ni chanjo ya kwanza kuwasili nchini humo.

Chanjo hiyo inatarajiwa kutolewa kwa wafanyakazi walio mstari wa mbele wanaopambana na virusi vya corona kwa mujibu wa wizara ya afya.

Taifa hilo la Afrika ya kati limeathirika kwa kiwango cha juu katika wimbi la pili la janga la virusi vya corona.

Wizara ya afya ya Cameroon, mpaka sasa imeripoti maambukizi 61,700 na vifo 919 toka mlipuko kuanza.

Takwimu za shirika la habari la Reuters zinaonyesha kwa wastani vifo 53 hutokea kwa siku nchini Cameroon.

Katika taarifa yake ya Ijumaa, wizara ya afya imeeleza kwamba dozi hizo za chanjo zitasaidia nchi hiyo, ambayo bado haijaanza kampeni yake ya chanjo.

Vilevile Cameroon inatarajia kupata chanjo kutoka COVAX ambao ni mpango wa kusaidia chanjo ya Covid-19 kwa nchi masikini.

XS
SM
MD
LG