Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:12

COVID-19 : WHO yatoa wito nchi tajiri kuchangia chanjo


Tedros Adhanom Ghebreyesus
Tedros Adhanom Ghebreyesus

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani – WHO Ijumaa ametoa wito kwa dunia kuchangia chanjo ya kuzuia virusi vya Corona kwa nchi zenye kipato cha chini akisema kuwa zinahitajika dozi milioni 10 katika program ya chanjo inayosimamiwa na WHO.

Amesema COVAX ipo tayari kusambaza chanjo, lakini hiana dozi za kutosha kutekeleza mpango huo. Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa Habari kwa njia ya mtandao akiwa Geneva.

COVAX ni programu ya usambazaji chanjo ya Covid-19 duniani yenye lengo la kuhakikisha dunia inafikia chanjo na hasa katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati.

Miongoni mwa mambo ambayo WHO imeomba pia ni kuhakikisha program ya COVAX inafadhiliwa ili iweze kusambaza chanjo katika nchi husika .

Hadi sasa kupitia program ya COVAX zaidi ya dozi milioni 31 za chanjo zimesambazwa katika nchi 57.

Wakati huohuo chuo kikuu cha Johns Hopkins hapa Marekani kimeripoti maambukizi zaidi ya milioni 126 kote ulimwenguni.

Marekani ina kesi nyingi kuliko nchi nyingine , kukiwa na maambukizi zaidi ya milioni 30.1 ikifuatiwa na Brazil yenye maambukizi milioni 12.4 na India ni milioni 11.9.

XS
SM
MD
LG