Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:10

COVID-19 : Maambukizi Mexico yaongezeka kwa asilimia 60


Ramani ya Marekani na Mexico ikionyesha mpaka wa San Diego/Tijuana
Ramani ya Marekani na Mexico ikionyesha mpaka wa San Diego/Tijuana

Mexico imetangaza idadi mpya ya maambukizi kutokana na virusi vya corona kuongezeka kwa asilimia 60 na kwa hivyo kuwa taifa la pili kwa wingi wa maambukizi baada ya Marekani huku likichukuwa nafasi iliyokuwa imeshikiliwa na Brazil.

Takwimu hizo mpya zina semekana kutisha ikizingatiwa kuwa idadi ya watu nchini Mexico ni ndogo ikilinganishwa na ile ya Marekani na Brazil. Wizara ya afya ya taifa hilo Jumapili imetoa takwimu ya vifo zaidi ya 321,000 kutokana na virusi vya Corona.

Marekani kufikia sasa imetangaza zaidi ya vifo 549,000 huku Brazil ikiwa na zaidi ya 312,000 kutokana na janga hilo kwa mujibu wa ripoti kutoka chuo kikuu cha Johns Hopkins cha hapa Marekani.

Wachambuzi wa masuala ya afya wa Mexico wamesema kuwa idadi ya vifo kutokana na corona huenda ikawa kubwa zaidi ya ilivyoripotiwa kutokana na kuwa kuna watu wengi waliofia nyumbani baada ya mfumo wa afya kuelemewa.

Ingawa zoezi la kutoa chanjo nchini Marekani limeendelea vizuri, idadi ya maambukizi kutokana na virusi hivyo imeendelea kubaki juu.

Mshauri mkuu wa maswala ya afya kwenye ikulu ya Marekani Anthony Fauci amesema kuwa huenda hali hiyo imechochewa na kuondolewa mapema kwa baadhi ya tahadhari zilizokuwa zimewekwa.

XS
SM
MD
LG