Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:14

Kifua kikuu chapata changamoto kutokana na uwepo wa Covid-19


Mgonjwa wa kifua kikuu
Mgonjwa wa kifua kikuu

Machi 24 kila mwaka ni siku ya kifua kikuu duniani.

Madaktari wanaonya kuwa maendeleo yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu yamerudi nyuma kwasababu ya janga la virusi vya corona.

Kifua kikuu kimeua watu milioni 1.4 kote duniani mwaka 2019.

Mwaka 2020, janga la virusi vya corona lilielemea huduma za afya kote duniani.

Nchi tisa zenye viwango vya juu vya TB, miongoni mwao ni Afrika Kusini, India, Pakistan na Indonesia, ambapo utambuzi na kutibu ugonjwa huo kumeshuka kwa kiwango cha wastani wa asilimia 23.

Takwimu hiyo ni kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na Stop TB Partnership, shirika lisilo la kiserikali ambalo linapata msaada wa Umoja wa Mataifa huko Geneva.

Wanasema mapambano dhidi ya TB yamerudi nyuma kwa takriban miaka 12.

Dr, Lucica Ditiu, mkurugenzi mtendaji wa Stop TB Partnership amesema.

“Imekuwa na athari kwa kazi zote ambazo tumejaribu kufanya, lakini pia kwa ufadhili ambao tumetumia, juhudi zote za kila mtu, kimsingi tumerudi nyuma, tumerejea kule ambako tulikuwa hapo awali.”

Kama Covid 19, kifua kikuu ni ugonjwa unaoathiri mapafu, na unaosababishwa na bakteria, badala ya virusi.

“Watu wengi ambao wanakabiliana na TB, madaktari, wauguzi, wafanyakazi wa huduma za afya, walibadilishwa na kuondolewa kwenye TB na kupelekwa kushughulikia Covid.” Alisema.

Wadi katika hospitali ambazo zilitumiwa na wagonjwa wa TB haraka zilibadilishwa na kuwa vitengo vya dharura kwa ajili ya Covid 19.

Wakati nchi zikiweka amri ya kufunga baadhi ya shughuli ili kupambana na janga, utambuzi kuhusu TB na matibabu yake kwa mara nyingine yalipunguza kasi.

Hiyo ina maana wagonwja wengi wanakuwa na maambukizi makubwa pale wanapofika kwenye kliniki au hospitali.

Ditiu anasema kuna fursa ya kurejesha maendeleo yaliyopotea. Janga la virusi vya corona limelazimisha watoa huduma za afya na jamii kuwa karibu sana. Ukichanganya uimaji, kuwafualitia wat una matibabu kwa Covid na TB, maradhi yote mawili yanaweza kushughulikiwa kwa wakati mmoja.

Wanasayansi wanasema uwekezaji wa haraka pia unahitaji katika chanjo mpya ya TB na matibabu.

XS
SM
MD
LG