Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:58

Misri yasema meli iliyokwama Mfereji wa Suez imeanza kusogea


Meli ya Ever Given, ikionekana imeanza kusogea kwenye Mfereji wa Suez, Misri, Machi 29, 2021.
Meli ya Ever Given, ikionekana imeanza kusogea kwenye Mfereji wa Suez, Misri, Machi 29, 2021.

Mamlaka ya safari za meli kwenye Mfereji wa Suez nchini Misri, SCA, imesema mapema Jumatatu kuna matumaini ya kurejea kwa safari za meli baada ya kuonekana kwa dalili za kusogea meli iliyokwama na kuziba mfereji huo kwa karibu wiki moja sasa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo Osama Rabie, kuna takriban meli 369 zinazo subiri kutumia mfereji huo zikiwa zimebeba bidhaa muhimu kama vile mafuta na gesi ya kupikia.

Rabie ameiambia televisheni ya taifa ya Misri kwamba kuna uwezekano wa kurejeshwa kwa shughuli za kawaida baadaye leo.

Ameongeza kusema kuwa huenda ikachukua muda wa takriban siku tatu kupisha meli zilizo songamana baada ya kuikwamua meli hiyo Ever Given iliyobeba zaidi ya tani 400,000 za mizigo.

Kampuni inayo endesha shuguli za meli hiyo ya Bernhard Schulte imesema kuwa operesheni za kuikwamua meli hiyo zinaendelea.

Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha meli hiyo ikianza kufungua sehemu ya mfereji huo huku meli za uokozi zilizoko karibu zikipiga ving’ora kuashiria matumaini.




XS
SM
MD
LG