Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:18

Tanzania : Rais aitaka Takukuru kuondoa kesi za kubambikizwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipokea taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020 kutoka kwa Mkuu wa Taasisi hiyo Brigedia Jenerali John Mbungo Machi 28,2021 Ikulu Chamwino, Dodoma, Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipokea taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020 kutoka kwa Mkuu wa Taasisi hiyo Brigedia Jenerali John Mbungo Machi 28,2021 Ikulu Chamwino, Dodoma, Tanzania.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuharakisha kesi, kuondoa kesi zisizo na msingi na za kubambikizwa ili kuondokana na idadi kubwa ya kesi ambazo Serikali inashindwa.

Rais Samia ameyasema hayo Jumapili, baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Rais amesema amefurahishwa na tathmini ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kiwango cha asilimia 89.8 ya malengo yaliyopangwa na hivyo kuitaka taasisi hiyo ijipime zaidi na kuongeza juhudi hasa katika kuharakisha kesi kusikilizwa.

“Ningeomba ziharakishwe, ukiangalia idadi ya kesi mlizo nazo na zile ambazo mmeshazifanyia kazi zipo mahakamani karibu ni nusu kwa nusu. Naomba kuliko kujirundikia kesi nawaomba zile ambazo hazina misingi na haziwapi uhalali wa kuzipeleka mahakamani basi mzifute ili muondoe huo mzigo,” amesema.

Rais Samia ameitaka Takukuru kuendelea kusimamia kesi zenye uhalali kwa kuzifanyia kazi kwa kasi na kuzifikisha kunakotakiwa, huku ikipunguza idadi ya kesi ambazo wanashindwa mahakamani.

“Hapa kuna kesi tunazo shindwa na hizi hazikuwa na misingi mizuri au zilikuwa za kubambikizwa yote haya yapo! Kwa hiyo nakuomba Mkurugenzi zile ambazo huna misingi mizito ya kuweza kushinda zifute kabla hujazipeleka huko kila siku kusema kuna kesi tumeshindwa hazina tija kwa Serikali.

XS
SM
MD
LG