Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:20

Watanzania wanatakiwa kuendelea kuimarisha uzalendo walionao


Sanduku lililohifadhi mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli
Sanduku lililohifadhi mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli

Marais wastaafu wa Tanzania ni miongoni mwa viongozi mbali mbali wanaotoa wito kwa watanzania kushikamana kudumisha umoja ili kusonga mbele kukuza maendeleo ya taifa hilo baada ya kifo cha Magufuli

Marais wastaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete pamoja na viongozi waandamizi katika serikali na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wanatoa wito kwa watanzania kuendelea kuimarisha uzalendo na fikra alizokuwa nazo hayati John Pombe Magufuli, ili kufanikisha Tanzania kukua kimaendeleo.

Wito huo umeelezwa wakati viongozi hao wakisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar Es Salaam kufuatia kifo cha Magufuli kilichotokea Machi 17 katika hospitali ya Mzena mjini Dar es Salaam mahala ambako alilazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Mazishi ya Magufuli yanatarajiwa kufanyika Machi 26 nyumbani kwao Chato katika mkoa wa Geita.

XS
SM
MD
LG