Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:35

Rais Samia aongoza kuuaga mwili wa hayati Magufuli Dar es Salaam


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiuaga mwili wa hayati John Pombe Magufuli. Picha na Ikulu.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiuaga mwili wa hayati John Pombe Magufuli. Picha na Ikulu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Samia Suluhu Hassan, Jumamosi ameongoza viongozi na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Kulingana na vyanzo vya habari nchini Tanzania katika zoezi hilo viongozi mbalimbali, wakiwemo wabunge, mawaziri na wananchi, wamejitokeza kumuaga hayati Magufuli aliyefariki Machi 17 mwaka 2021, mjini Dar es alaam kutokana na tatizo la moyo.

Vilio na majonzi vilitawala katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, ambapo zoezi hilo la kutoa heshima za mwisho linaendelea kufanyika.

Mwili wa Hayati Magufuli ukwasili Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.
Mwili wa Hayati Magufuli ukwasili Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.

Hapo mwanzoni kabla ya shughuli hiyo ya kuuaga mwili wa Magufuli haijaanza, kulitanguliwa na ibada ya misa takatifu .

Jiji la Dar es Salaam litakamilisha zoezi la kuaga mwili wa hayati Magufuli Jumapili, ambapo siku ya Jumatatu viongozi wa nchi mbalimbali, wawakilishi wa jumuiya za kimataifa, mabalozi na wananchi wa mikoa ya kanda ya kati watashiriki kuuaga mwili wa marehemu.

Watafuatiwa na mikoa mingine na kisha kuzikwa siku ya Ijumaa ya Machi 26 nyumbani kwa marehemu Chato Geita, Kaskazini Magharibi mwa taifa hilo.

XS
SM
MD
LG