Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:26

Maelfu Wajitokeza, kumwaga hayati Rais Magufuli Zanzibar


Makamanda wa JWTZ wakipiga Saluti mara baada ya kuweka Jeneza lenye Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika chumba maalumu kwa ajili ya shughuli ya kuagwa na viongozi mbalimbal
Makamanda wa JWTZ wakipiga Saluti mara baada ya kuweka Jeneza lenye Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika chumba maalumu kwa ajili ya shughuli ya kuagwa na viongozi mbalimbal

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli umeagwa Jumanne visiwani Zanzibar ambako wananchi waliojitokeza kwa wingi wakiongozwa na rais wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Mwinyi na viongozi wengine wa serikali.

Mwili wa Dkt. Magufuli ulipitishwa katika barabara za baadhi ya mitaa kuelekea Uwanja wa Amaan Zanzibar ambapo ibada ya kuagwa ilifanyika.

Akimzungumzia wasifu wa Hayati Magufuli, Rais Mwinyi amesema Wazanzibari wameonyesha upendo wa kuthamini mchango wa Rais huyo wa awamu ya tano wa Tanzania kwa kutaka kumuaga katika ardhi ya Zanzibar

Dk. Hussein amesema wazanzibar watamkumbuka hayati Magufuli kwa jitihada zake za kulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, pamoja na Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Awali Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya mazishi, waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa ratiba ya maombolezo na kuagwa kwa hayati Magufuli mara baada ya mwili kuondoka visiwani zanzibar.

Hayati Magufuli aliyezaliwa Chato mwaka 1959, anatarajiwa kuzikwa Ijumaa wiki hii Wilayani Chato, mkoani Geita.

XS
SM
MD
LG