Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antonu Blinken, ameelekea Brussels, Jumatatu jioni ikiwa ni ziara yake ya pili ndani ya kipindi cha wiki moja kukutana na washirika wa NATO wakati maamuzi yakihitajika kufanyika kuhusiana na vita vya Afghanistan.
Blinken pia anatarajiwa kujadili kuongeza hatua ya kidiplomasia zenye kuungwa mkono na umoja wa Ulaya katika kuyarejesha makubaliano ya nyuklia na Iran, na wasiwasi unaoongezeka wa Russia ambayo inaendelea kujengo himaya ya kijeshi karibu na Ukraine.
Ataanza mazungumzo leo hii mjini Brussels, na ataungana na waziri wa ulinzi Lloyd Austin ambaye anatembelea washirika muhimu ikiwemo Ujerumani pamoja na Israel, ambalo ni taifa muhimu katika diplomasia na Iran.
Rais wa Marekani, Joe Biden ameapa kumaliza vita vya muda mrefu vya Marekani ndani ya mwaka mmoja lakini amesema kwamba siku ya mwisho ya tarehe mosi May haina uhalisia.