Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:45

Siku 100 za Biden, washirika Ulaya waona mabadiliko katika uhusiano na Washington


Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden.

Wiki hii wakati utawala wa Biden ukiadhimisha siku 100 za urais wake washirika wa Ulaya wanaona mabadiliko katika uhusiano muhimu na Washington. Henry Ridgwell anaripoti kutoka London juu ya jinsi utawala mpya unavyoangaliwa kutoka upande mwingine wa bahari ya Atlantiki

Hata kwa njia ya video, dalili za mabadiliko katika uhusiano wa nchi za ulaya na marekani ziliweza kuonekana. Urais wa Joe Biden nchini marekani umeleta mabadiliko makubwa katika ushirikiano huo na Ulaya imepokea vizuri mabadiliko hayo, anasema mchambuzi Leslie Vinjamuri.

Marekani imejiunga tena na Shirika la Afya Duniani -WHO na makubaliano juu ya hali ya hewa ya Paris. Waziri wa mambo ya nje wa Biden ametembelea Brussels mara mbili akielezea msaada kwa NATO na Umoja wa Ulaya.

Washington pia imejiunga na mazungumzo yenye lengo la kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015, ambayo Ulaya inaona kama ushindi wa diplomasia yake. Utawala wa zamani wa Trump ulijiondoa kutoka kwenye makubaliano hayo, ukiona kuwa yana kasoro kubwa.

Biden pia amechukua mbinu mpya na wapinzani wa Marekani , akimtaja mwenzake wa Russia Vladimir Putin kuwa muuaji na kuweka duru mbili za vikwazo kwa Moscow.

Wakati huo huo, Russia imetuma zaidi ya wanajeshi laki moja kwenye mpaka wa Ukraine inayoonekana kwa kiasi kikubwa kama jaribio kwa Rais Biden.

Huko Moscow, Warussia ambao walizungumza na VOA wamesema uhusiano na Marekani umedorora chini ya Rais Biden.

Kwa China, utawala wa Biden umeishutumu Beijing kwa kutekeleza vitendo vya mauaji ya halaiki dhidi ya idadi ya watu wa Uyghur katika mkoa wa Xinjiang. China inakanusha mashtaka hayo.

Wiki hii, rais wa Marekani alitambua mauaji ya Uturuki ya Waarmenia karibu milioni moja wakati wa Vita vya dunia vya kwanza kama mauaji ya kimbari.

Kwa sasa, wachambuzi wanasema Biden bado anafurahiya wakati wa sherehe na washirika wa Ulaya.

XS
SM
MD
LG