Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:21

Ndege maalum iliyobeba raia wa Afghanistan yawasili Marekani


Mfano wa ndege maalum iliyobeba raia wa Afghanistan waliowasili Marekani
Mfano wa ndege maalum iliyobeba raia wa Afghanistan waliowasili Marekani

Maafisa wa White House walitangaza hivi karibuni “Operesheni ya hifadhi ya washirika” itawaondoa wakalimani wa Afghanistan na  watu wengine ambao waliisaidia serikali ya Marekani wakati wa vita pamoja na familia zao ambazo hivi sasa zinahofia hatua ya kulipiziwa kisasi kutoka kwa Taliban

Ndege maalumu kwa ajili ya raia wa Afghanistan 200 wanaostahili “hadhi maalumu ya uhamiaji (SIV)”, iliwasili Marekani Ijumaa kama sehemu ya operesheni ya kuwaondoa wale waliotoa msaada kwa serikali ya Marekani.

Maafisa wa White House walitangaza “Operesheni ya hifadhi ya washirika” hapo Julai 14 wakisema itawaondoa wakalimani wa Afghanistan na watu wengine ambao waliisaidia serikali ya Marekani wakati wa vita pamoja na familia zao ambazo hivi sasa zinahofia hatua ya kulipiziwa kisasi kutoka kwa Taliban.

Naibu mshauri mwandamizi wa usalama wa ndani Russ Travers wa baraza la usalama la taifa aliwaambia waandishi wa habari kwamba “ndege hiyo inawakilisha kutimiza ahadi ya Marekani, na inaheshimu utumishi jasiri kwa wa-Afghanistan katika kusaidia kuunga mkono operesheni zetu”.

XS
SM
MD
LG