Wapiga kura wengi walijitokeza katika mji mkuu, Lusaka, na maeneo mengine katika taifa hilo la kusini mwa Afrika.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa uchaguzi mkuu huo ulio na ushindani mkali ambao rais aliyepo madarakani na mpinzani wake mkuu wamesema ni mtihani kwa uthabiti wa demokrasia ya taifa hilo.
Zaidi ya watu milioni 7, au zaidi ya asiliomia 83 ya wapiga kura wanaostahiki nchini Zambia, wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa rais na wabunge katika vituo zaidi ya 12,000, kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Zambia.