Marehemu Kaunda alilazwa katika hospitali hiyo akitibiwa ugonjwa wa nimonia, mtoto wake Kambarage alisema Jumatano.
Kaunda alitawala Zambia tangu mwaka 1964, wakati taifa hilo la kusini mwa Afrika lilipopata uhuru wake kutoka kwa Uingereza, hadi 1991.
Pia hayati Kaunda baadaye alikuwa mmoja wa wanaharakati waliojitolea zaidi Afrika dhidi ya Virusi vya Ukimwi.
Nina huzuni kuwajulisha tumempoteza Mzee wetu. Tumuombee, Kambarage alisema kwenye ukurasa wa Facebook wa hayati baba yake.
Kaunda alikuwa akichukuliwa kama mmoja ya watu wa mwisho kwenye kizazi cha mashujaa wa uhuru barani Afrika. Alitawala Zambia kuanzia mwaka 1964 hadi 1991.