Hamdok amesema makundi yaliyofanikisha mapinduzi ya kumuondoa rais wa muda mrefu wa Sudan, Omar al Bashir, mwaka 2019 lazima yashikamane kwa kufanya mazuri kwa Sudan.
Katika hotuba ya televisheni amejaribu kuwahakiishia wananchi wa Sudan kwamba mabadiliko magumu na yenye matarajio makubwa yaliyoanzishwa na serikali yake ya mpito yatabadilisha uchumi.
Saa kadhaa mapema, Jumatano mazungumzo ya amani baina ya serikali na makundi makubwa ya waasi yaliahirishwa ili kutoa nafasi kwa pande zote mbili kupitia mchakato na kutafuta suluhu.
Habari inatokana na vyanzo mbalimbali