Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:53

Sudan yaridhia mkataba wa UN wa haki za wanawake kwa masharti


Wanawake wa Sudan wakiimba wakati wa maandamano ya kutetea demokrasia nchini humo.
Juni 30, 2020.
Wanawake wa Sudan wakiimba wakati wa maandamano ya kutetea demokrasia nchini humo. Juni 30, 2020.

Baraza la mawaziri la Sudan wiki hii liliidhinisha mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wanawake. Lakini wakosoaji wanaona baraza la mawaziri lilikataa kuthibitisha haki fulani ambazo zingewapa wanawake wa Sudan usawa wa kweli wa kisheria na wanaume.

Baraza hilo la Mawaziri la Sudan limeidhinisha Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa 1979 juu ya Kutokomeza aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW).

Walakini, baraza hilo ambalo wajumbe wake wengi ni wanaume lilikataa kuidhinisha wazo kwamba wanawake ni sawa na wanaume katika ngazi zote za kisiasa na kijamii na wana haki sawa katika ndoa, talaka na uzazi.

Vikundi vya haki za wanawake vilikosoa hali hiyo na kusema hawatakubali.

Mwishoni mwa mwaka 2018 na mapema 2019, wanawake wa Sudan walichukua majukumu makubwa katika maandamano ya umma dhidi ya Rais wa muda mrefu Omar al-Bashir, ambaye alitolewa mamlakani Aprili, 2019.

Mwaka jana, baadhi ya wanawake wa Sudan walipokea tuzo za kimataifa kwa kuhusika kwao katika mabadiliko ya kidemokrasia nchini humo.

XS
SM
MD
LG