Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 04:15

Watu angalau 36 wameuawa Darfur kusini na wengine wamejeruhiwa


Watoto wa kisudan wakiwa wamekaa pamoja kufuatia ghasia katika mkoa wa Darfur huko Sudan, Feb. 2, 2021.
Watoto wa kisudan wakiwa wamekaa pamoja kufuatia ghasia katika mkoa wa Darfur huko Sudan, Feb. 2, 2021.

Ghasia zilitokea kati ya wanachama wa makundi ya Fellata na Taisha katika eneo la Um Dafuq, shirika la habari la SUNA liliripoti. Mkazi mmoja alisema mapigano yalitokea Jumamosi kufuatia mzozo wa ardhi

Watu angalau 36 waliuawa na 32 walijeruhiwa katika mapambano katika jimbo la Darfur Kusini nchini Sudan, shirika la habari la SUNA liliripoti Jumapili.

Ghasia zilitokea kati ya wanachama wa makundi ya Fellata na Taisha katika eneo la Um Dafuq, shirika la habari la SUNA liliripoti. Mkazi mmoja alisema mapigano yalitokea Jumamosi kufuatia mzozo wa ardhi.

Usalama umekuwa mbaya katika miezi ya karibuni huko Darfur, licha ya makubaliano ya amani yaliyotiwa Saini kati ya mamlaka ya mpito ya Sudan na baadhi ya makundi ya uasi mwishoni mwa mwaka 2020.

Walinda amani wa UN na Umoja wa Afrika (UNAMID) wakiwa Darfur kusini Dec. 31, 2020.
Walinda amani wa UN na Umoja wa Afrika (UNAMID) wakiwa Darfur kusini Dec. 31, 2020.

Kikosi cha pamoja cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kilisitisha doria Januari mosi, kabla ya kuondoka kwake, huku jeshi la taifa la Sudan limeahidi kuleta uthabiti katika eneo lake la Darfur.

Mzozo ambao uliongezeka kote Darfur kutoka mwaka 2003, ulipungua kwa kiasi kikubwa, lakini watu takribani milioni 1.5 bado wamekoseshwa makazi ndani ya nchi na pia milipuko ya ghasia imekuwa jambo la kawaida tangu mwaka 2020.

XS
SM
MD
LG