Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:48

Sudan inatuma ujumbe kwa Israel kuimarisha uhusiano wa nchi zao


Ramani ya Sudan
Ramani ya Sudan

Chanzo kimoja ambacho hakikuweza kutambuliwa kwa jina au utaifa, kilisema ujumbe wa Sudan utajumuisha maafisa wa usalama na upelelezi lakini tarehe maalumu kwa ziara ya wiki ijayo bado haijajulikana

Sudan inapanga kutuma ujumbe rasmi wa kwanza kwa Israel wiki ijayo ili kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili ambao ulianzishwa mwaka jana chini ya upatanishi wa Marekani, vyanzo viwili vimesema Jumanne.

Chanzo kimoja ambacho hakikuweza kutambuliwa kwa jina au utaifa, kilisema ujumbe wa Sudan utajumuisha maafisa wa usalama na upelelezi. Tarehe maalumu kwa ziara ya wiki ijayo bado haijajulikana, chanzo hicho kiliongeza.

Wasemaji wa serikali za Sudan na Israel hawakuwa na maoni ya mara moja juu ya ziara hiyo.

Sudan iliungana na umoja wa falme za kiarabu, Bahrain na Morocco kukubali kuelekea uhusiano wa kawaida na Israel katika mikataba ya mwaka 2020 ya Abraham Accords iliyosimamiwa na utawala wa Trump. Utawala wa Biden umeahidi kufuata ufikiaji huo.

Urekebishaji huo unaonekana nchini Sudan kama mpango unaoongozwa na wanajeshi, ambao umekaribisha ziara za maafisa wa Israel katika miezi ya hivi karibuni. Kwa hatua inayohusiana, baraza la mawaziri la Khartoum lilipiga kura wiki iliyopita kufuta sheria yam waka 1958 ambayo ilikataza uhusiano wa kidiplomasia na biashara na Israel.

XS
SM
MD
LG