Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:20

Serikali ya Marekani imenunua dozi milioni 200 nyingine za Moderna dhidi ya COVID-19


Chanjo ya Moderna inayotumika dhidi ya COVID-19
Chanjo ya Moderna inayotumika dhidi ya COVID-19

Mei 2021 kampuni ya Moderna ilitangaza chanjo yake ilikuwa salama na yenye ufanisi kwa watu wa miaka 12 hadi 17 na iliomba idhini kutoka idara inayohusika na kiwango cha chakula na dawa Marekani (FDA) kwa chanjo hiyo kutumika kwa watoto

Kampuni inayotengeneza chanjo ya Moderna yenye makao yake Marekani ilisema Jumatano kwamba serikali ya Marekani imenunua dozi milioni 200 nyingine za chanjo yake ya COVID-19 ikijumuisha jumla ya dozi za Moderna milioni 500 ilizoahidi kutoa.

Katika kutolewa kwa dozi hizo hapo Jumatano kampuni hiyo iliyopo Massachusetts ilisema maagizo ya serikali ya Marekani yanajumuisha dozi milioni 110 zilizotarajiwa kutolewa katika robo ya nne ya mwaka huu wa 2021 na dozi milioni 90 zilizotarajiwa kutolewa katika robo ya kwanza ya mwaka 2022.

chanjo ya Moderna dhidi ya COVID-19
chanjo ya Moderna dhidi ya COVID-19

Kufikia Jumatatu kampuni inasema imesambaza dozi milioni 217 za chanjo hiyo kwa serikali ya Marekani. Katika taarifa hiyo afisa mtendaji mkuu wa Moderna, Stephane Bancel, alisema kampuni hiyo inathamini ushirikiano na serikali ya Marekani kwenye dozi za ziada akiongeza kuwa itaweza kutumika kwa program ya chanjo inayoendelea, au kwa watoto, au pengine dozi ya kuimarisha chanjo katika siku zijazo.

Mei mwaka 2021 kampuni ya Moderna ilitangaza chanjo yake ilikuwa salama na yenye ufanisi kwa watu wa miaka 12 hadi 17 na iliomba idhini kutoka idara inayohusika na kiwango cha chakula na dawa Marekani (FDA) kwa chanjo hiyo kutumika kwa watoto.

XS
SM
MD
LG