Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:01

Ufaransa yaipa Uganda dozi 175,200 za chanjo, wakati maambukizi yakiongezeka


Chanjo aina ya AstraZeneca
Chanjo aina ya AstraZeneca

Uganda imepokea dozi 175,200 za chanjo za COVID -19 aina ya AstraZeneca zilizotolewa msaada na Ufaransa.

Chanjo hizo zimewasili wakati ambapo taifa hilo la Afrika Mashariki linakabiliwa na upungufu wa chanjo, huku maambukizi ya ugonjwa huo yakizidi kuongezeka.

Chanjo hizo zilitolewa chini ya mpango wa COVAX kulingana na msemaji wa Wizara ya Afya.

Hii ni mara ya tatu kwa Uganda, kupokea msaada wa chanjo, tangu ilipopata dozi 864,000, mwanzoni mwa mwezi Machi, mwaka 2021, iliyotengenezwa na Taasisi ya Serum, ya India.

Pia msaada mwingine wa dozi laki moja, uliotolewa na taifa hilo la kusini mwa Asia.

Wizara ya Afya ya Uganda Jumatano ilisema watu 49 zaidi walikufa kutokana na maambukizi ya Covid-19, idadi kubwa zaidi kuwahi kuripotiwa, kwa siku moja, nchini humo.

Maafisa wa afya wamesema jumla ya idadi ya vifo, ilikuwa imefikia 508, tangu ugonjwa huo kuripotiwa, mwezi Machi, mwaka 2020.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali

XS
SM
MD
LG