Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:21

COVID-19 : Museveni kuzungumzia mikakati ya kupambana na ongezeko la maambukizi


Rais Yoweri Museveni (Twitter/Mbulamatari ya Ouganda)
Rais Yoweri Museveni (Twitter/Mbulamatari ya Ouganda)

Rais wa Uganda Yoweri Museveni Jumapili anatarajiwa kulihutubia taifa kuelezea mikakati ya serikali yake katika kupambana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona.

Kupitia ujumbe wa Twitter, Museveni amewataka raia wote wa Uganda kutazama au kusikiliza hotuba yake kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuanzia mwendo wa saa mbili usiku.

“Nitalihutubia taifa hii leo juu ya maazimio na hatua zilizopitishwa na tume ya kitaifa ya kukabiliana na COVID-19, alisema Museveni. Wakati wa hotuba yake juzi Ijumaa, rais huyo alisema kwamba Uganda inaingia katika wimbi la tatu la maambukizi ya Corona.

Hotuba ya leo inajiri huku taifa hilo la Afrika Mashariki likiwa limerekodi idadi kubwa zaidi ya maambukizi wiki hii, jambo ambalo limepelekea kuwepo wasiwasi mkubwa kati ya raia na maafisa wa serikali.

Kufikia Jumapili, Uganda imeripoti jumla ya maambukizi 51, 676 huku watu 374 wakifariki kutokana na ugonjwa huo. Katika nchi yenye jumla ya wakazi milioni 41, ni takriban watu 750,000 tu ambao wamepata chanjo ya COVID-19.

Wachambuzi wanasema kwamba huenda rais Museveni akatangaza masharti makali zaidi, katika juhudi za kukabiliana na ongezeko hilo, la maambukizi.

XS
SM
MD
LG