Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:15

Watu wasiopungua 10 wafariki katika ajali ya barabarani Uganda


Ramani ya Uganda
Ramani ya Uganda

Watu wasiopungua kumi na watatu wamethibitishwa kufariki katika ajali ya barabarani nchini Uganda Alhamisi asubuhi.

Kwa mujibu wa maafisa wa polisi nchini humo, ajali hiyo, iliyohusisha magari mawili, ilitokea kwenye barabara inayounganisha barabara kuu ya kutoka Masaka kwenda Mbarara katika mji wa Masaka.

Mashahidi walionukuliwa na gazeti la Daily Monitor wamesema kwamba basi lililohusika kwenye ajali hiyo, lilikuwa likiendeshwa kwa kasi kubwa.

Wameeleza kuwa basi hilo baada ya kugonga taxi iliyojaa abiria, halikusimama.

Polisi wamesema watu kadhaa waliokuwa kwenye taxi hiyo, walijeruhiwa na kupelekwa hospitali iliyo karibu na eneo la tukio hilo.

XS
SM
MD
LG