Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:37

Kenya yarekodi ongezeko la mapato ya nje kwa zaidi ya bilioni 45/-


Ramani ya Kenya na Tanzania
Ramani ya Kenya na Tanzania

Mapato ya Kenya katika masoko ya nje yameongezeka kwa zaidi ya shilingi bilioni 45 mwaka 2020, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 7.8 kufikia Disemba 2020, licha ya kuwepo na hofu iliyosababishwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Kenya imepata soko kubwa nchini Uganda, ikifuatiwa na Pakistan, Uingereza na Marekani huku kiasi hicho cha mauzo kikipungua katika soko la Tanzania kwa zaidi ya shilingi bilioni mbili, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kuhamasisha uuzaji wa bidhaa za Kenya nje ya nchi, KEPROBA.

Kenya ilikadiria kuwa mapato yake katika masoko ya nje yangepungua kwa zaidi ya asilimia 20% mwaka 2020 kwa sababu ya vikwazo vilivyosabishwa na janga la virusi vya Corona.

Thamani ya mauzo ya nje mwaka 2020 imefikia shilingi bilioni 642 ikilinganishwa na shilingi bilioni 595 mwaka 2019.

Soko la Uganda

Mauzo ya nje kutoka Kenya yamepata soko kubwa nchini Uganda ikiwa ni shilingi bilion 8.42, Uingereza, Pakistan, Marekani, Sudan Kusini, Rwanda na Ujerumani.

Lakini, thamani ya mauzo hayo ilipungua, kwa zaidi ya shilingi bilioni 1 za Kenya, katika masoko ya Tanzania kwa zaidi ya shilingi bilioni 2.2 na masoko mengine kama vile Canada, Singapore, Saudi Arabia na Qatar.

Mauzo hayo yanajumuisha chai, kahawa, maua, mavazi, na chuma, bidhaa za tumbaku, mboga, matunda na dawa.

Masoko ya Chai

FILE — Kahawa ikiwa tayari kusafirishwa kutoka kwa wakulima nchini Kenya.
FILE — Kahawa ikiwa tayari kusafirishwa kutoka kwa wakulima nchini Kenya.

Mwaka 2020, bidhaa zilizonawiri katika masoko ya nje kama chai, maua, mafuta ya mboga, nafaka, bidhaa za tumbaku ziliizalishia Kenya zaidi ya shilingi bilioni mbili.

Lakini, licha ya kuwepo kwa virusi vya Corona, mbona mauzo ya Kenya nje ya nchi yakaongezeka kiwango hiki? Swali hili analijibu mchumi Isaac Tongola.

Tongola ameeleza kwa nini mauzo ya Kenya nje ya nchi yaliongezeka; anasema kuwa Uganda ni soko kubwa la Kenya katika ukanda wa Afrika Mashariki, na serikali mbili ziliweka makubaliano ya kuimarisha biashara licha ya changamoto zilizopo.

“Kwa upande mwingine, uagizaji jumla ulipungua kwa thamani ya shilingi trilioni 1.65 mwaka 2020 kutoka shilingi trilioni 1.81 mwaka 2019,” mchumi huyo wa Kenya ameongeza.

Uagizaji Bidhaa

Uagizaji bidhaa unajumuisha bidhaa za bei ya juu na bidhaa kwa matumizi ya viwandani kama vile bidhaa za mafuta ya petroli, mashine za viwandani, mafuta yasiyosafishwa ya mboga, chuma ghafi, na plastiki.

Naye Mchumi wa Kenya Charles Kariisa anaeleza kuwa licha ya kuwapo vikwazo vilivyosababishwa na janga la Corona, nchi zilitafuta njia mbadala za kufanya biashara ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi.

“Kenya imekuwa ikieleza kuwa biashara, uwekezaji na wafanyakazi walio na ujuzi ndio viungo muhimu katika juhudi zake za kukua kwa kasi kufikia uchumi wa viwanda na kipato cha kati ifikapo 2030,” ameeleza.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Kennedy Wandera, Kenya

XS
SM
MD
LG