Katika taarifa ya shirika hilo la kimataifa iliyowekwa kwenye tovuti yake leo Jumatano, IMF imesema Kenya ilikuwa ikikabiliwa na changamoto za kifedha kutokana na madeni iliyokuwa ikiyalipa.
Mkopeshaji huyo alisema Kenya ilijikuta katika dimbwi la deni baada ya janga la Covid-19 kuharibu uchumi wake.
Taasisi hiyo ya ukopeshaji wa kimataifa imesema kuwa changamoto zingine za kifedha ambazo Kenya inakabiliwa nazo, zilikuwa zimeainishwa katika bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2020/2021.
IMF inasema ina matumaini kuwa uchumi wa Kenya utaimarika mara tu hali ngumu ya Covid-19 itakapodhibitiwa.
Kauli yake inajiri siku chache baada ya baadhi ya raia wa Kenya kuitaka taasisi hiyo kusita kuikopesha pesa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta, kwa madai ya ubadhirifu wa fedha katika taifa hilo la Afrika Mashariki.