Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:53

Zambia kufanya uchaguzi Alhamisi


Wafuasi wa chama tawala cha Zambia kwenye picha ya awali ya kampeni
Wafuasi wa chama tawala cha Zambia kwenye picha ya awali ya kampeni

Mji wa mkuu wa Lusaka, Zambia umejawa na mabango ya kampeni wakati taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika Alhamisi , ukielezewa ni wenye ushindani mkali.

Ripoti zinasema kuwa wanajeshi wamepelekwa kwenye maeneo tofauti ya nchi ili kutuliza hali baada ya ghasia kuzuka kati ya wafuasi wa chama cha Rais Edgar Lungu cha Patriotic Front, na kile cha upinzani cha UPND chake Hakainde Hichilema.

Rais Edgar Lungu kwa mara nyingine tena atamenyana na Hichilema ambaye ni mpinzani wake wa muda mrefu kwenye zoezi la Alhamis ambalo huenda likavutia vijana wengi, licha ya hali ngumu ya kiuchumi wanayopitia, wakati taifa hilo likisubiri kukombolewa kutokana na madeni mengi iliyonayo.

Wawekezaji wanafuatilia kwa karibu sana uchaguzi huo hasa ikizingatiwa kuwa Zambia ndiyo ndiyo mzalishaji mkuu wa shaba barani Afrika. Zambia pia Iilikuwa taifa la kwanza kutangaza kushindwa kutekeleza majukumu ya kulipa madeni yake Novemba baada ya janga la corona kuingia.

Thamani ya sarafu ya Kwacha inasemekana kushuka sana huku mfumuko wa bei ukiwa umevuka asilimia 20 wakati wa utawala wa Lungu. Imani ya wawekezaji pia inasemekana kushuka pakubwa wakati deni la nje likiwa takriban dola blioni 12 mwaka uliopita.

Lungu mwenye umri wa miaka 64 na ambaye amekuwa madarakani tangu 2015 anakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Hichilema anayejulikana pia kama HH, na ambaye ni mfanyabiashara mkubwa anayekosoa sera za uchumi za Lungu.

Zambia ina deni la zaidi ya dola bilioni 12 wakati ikitumia asilimia 30 hadi 40 ya mapato yake kulipia riba ya madeni hayo kulingana na kampuni ya kiuchumi ya S&P Global. Madeni yake yakilinganishwa na mapato ya ndani yalikuwa na tofauti ya asilimia 120 mwaka uliopita, kikiwa kiwango cha juu zaidi ambacho kikinasemekana kuwa vigumu kudhibiti.

Takwimu za maoni kabla ya uchaguzi kwa sasa hazitegemewi wakati wadadisi wakisema kuwa ushindani ulioko unakaribiana sana .Ghasia pia zimeongezeka katika kipindi cha kampeni wakati wafuasi wawili wa chama tawala wakisemekana kuuwawa kwa kukatwa kwa panga, hatua iliyopekea Lungu kutumia jeshi ili kutuliza hali.

XS
SM
MD
LG