Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:53

Uchaguzi Mkuu : Hesabu ya awali inaonyesha upinzani unaongoza Zambia


Mgombea Urais wa Chama cha Upinzani cha UPND Hakainde Hichilema alipokuwa akipiga kura Lusaka, Zambia, Agosti 12, 2021.
Mgombea Urais wa Chama cha Upinzani cha UPND Hakainde Hichilema alipokuwa akipiga kura Lusaka, Zambia, Agosti 12, 2021.

Kiongozi wa upinzani Zambia, Hakainde Hichilema, anaongoza katika hesabu ya awali katika uchaguzi wa rais nchini humo dhidi ya mpinzani wake wa muda mrefu ambaye pia ni Rais aliyepo madarakani Edgar Lungu, kulingana na matokeo ya kwanza yaliyotolewa na tume ya uchaguzi Jumamosi.

Lungu mwenye umri wa miaka 64 na amekuwepo madarakani tangu mwaka 2015, anakabiliwa na ushindani wa karibu sana dhidi ya Hichilema anayejulikana kama HH, mfanyabiashara anayekosoa usimamizi wa rais kwenye masuala ya uchumi ambao una matatizo.

Wawekezaji wanafuatilia kwa karibu matokeo ya uchaguzi wa Alhamisi ; kwenye nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambayo ina deni kubwa sana, na imeathiri sana janga la virusi vya corona tangu vilipoingia barani humo tangu mwezi November taifa limeshindwa kulipa madeni yake.

Msaada wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ambao tayari umekubaliwa kwa jumla, unasimamishwa hadi baada ya matokeo ya kura.

Hivyo hivyo katika kufanya mabadiliko katika madeni yake ambapo inaonekana ni mtihani wa mapema kwa mpango mpya wa ulimwengu kupunguza mzigo kwa nchi maskini.

XS
SM
MD
LG