Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:05

Mwanariadha wa Uingereza CJ Ujah matatani


Chijindu Ujah (Photo by Javier SORIANO / AFP)
Chijindu Ujah (Photo by Javier SORIANO / AFP)

Mwanariadha wa Uingereza CJ Ujah, ambaye alishinda medali ya fedha katika michezo ya Olimpiki kwenye mbio za mita 400 za kupokezana vijiti huko Tokyo, Alhamisi alisimamishwa kwa madai ya ukiukaji wa matumizi ya dawa za kusisimua misuli , Kitengo cha Uadilifu cha wanamichezo (AIU) kilitangaza.

Ikiwa kesi hiyo itathibitishwa, basi Ujah mwenye umri wa miaka 27 na timu ya Uingereza watavuliwa medali ya fedha walioshinda nyuma ya Italia huko Japan.

AIU ilisema kwamba Ujah aligundulika kuwa na utumiaji wa dawa iliyopigwa marufuku ostarine na S-23.

Ni dawa ambazo kwa kawaida hutumiwa kujenga misuli.

Pamoja na Ujah, mwanariadha wa Bahrain wa mbio za mita 1500 Sadik Mikhou, mrusha mikuki wa Georgia Benik Abramyan na mwanariadha wa Kenya Mark Otieno Odhiambo pia wamesimamishwa kwa muda kufuatia majaribio yaliyoonyesha matumizi ya dawa AIU imeongeza.

XS
SM
MD
LG