Ghasia hizo zinaonekana kuwa sehemu ya mzozo unaoendelea kutokana na kifo cha mwanafunzi raia wa Congo, aliyefariki katika rumande ya polisi nchini India wiki iliyopita.
Biashara kadhaa za raia wa India ziliporwa mjini Kinshasa wiki iliyopita, kufuatia kifo cha Joel Malu, mwanafunzi katika mji wa India wa Bangalore.
“Watu wasiokuwa na ustaarabu, haswa vijana, wamekuwa wakipora maduka na maghala yanayomilikiwa na raia wa India,”mkuu wa polisi mjini Kinshasa, Sylvano Kasongo amesema.
Polisi waliamata watu watatu na kupata marobota 40 ya nguo zilizoibwa, Kasongo ameongeza.Malu alikamatwa huko Bangalore tarehe 1 Agosti, kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya.
Polisi wa India walisema alilalamika kwamba ana maumivu ya kifua na alipelekwa hospitali, ambapo alifariki baadaye. Kifo chake kilizusha mapigano kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi wa Bangalore siku iliyofuata.