Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:27

Biden atetea uamuzi wa kuondoa wanajeshi Afghanistan


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden amesema anasimama ‘bila ya shaka’ kwa uamuzi wake wa kuondoa majeshi ya Marekani kutoka Afghanistan yakiwa matamshi yake ya kwanza tangu Taliban ilipochukua udhibiti kamili wa taifa hilo la Asia Kusini.

Katika hotuba yake kwa taifa kwa njia ya televisheni Jumatatu jioni akiwa White House, Biden amesema operesheni ya Marekani nchini Afghanistan “kamwe haikuwa kujenga taifa” na kusema tishio la ugaidi ambalo lililipeleka jeshi la Marekani katika nchi hiyo limevuka nje ya Afghanistan kwenye mataifa mengine.

Amekiri kwamba ushindi wa Taliban kote nchini Afghanistan umetokea, “kwa haraka sana kuliko ilivyotarajiwa.”

Hata hivyo, Biden amesema, ni kosa kuamuru wanajeshi wa Marekani kujihusisha katika mapambano zaidi, wakati wanajeshi wa Afghanistan hawako tayari kufanya hivyo.

“Kama kuna chochote,” amesema, “Maendeleo ya wiki iliyopita yanaimarisha” uamuzi wake wa kuondoa wanajeshi kutoka Afghanistan.

Biden alirejea White House kutoka Camp David Jumatatu, siku moja baada ya Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani kutoroka nchini wakati wapiganaji wa Taliban walipofika katika mji mkuu wa Kabul.

Biden amekuwa akitetea uamuzi wake wa kuondoa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini humo ifikapo Agosti 31.

“Mwaka mwingine mmoja, au miaka mingine mitano, uwepo wa jeshi la Marekani hautaleta tofauti kama jeshi la Afghanistan haliwezi, au haliko tayari kuilinda nchi yake,” Biden alisema katika taarifa yake Jumamosi. “Uwepo wa Marekani usio na muda katikati ya vita vingine vya wenyewe kwa wenyewe haukubaliki kwangu mimi.

Majeshi ya Marekani yamekuwepo Afghanistan kwa takriban miaka 20, marais wanne wa Marekani walikuwa madarakani. Biden alitangaza mwezi April kwamba wanajeshi wote wa Marekani watarejea nyumbani kutoka Afghanistan ifikapo mwisho wa mwezi Agosti, na kukataa pendekezo la Pentagon kwa Marekani kuwa na kikosi kidogo katika taifa hiyo.

Biden amesema kuwa hatapitisha jukumu la kuwarejesha nyumbani wanajeshi wa Marekani kwa rais wa tano.

Taliban ili zidisha mashambulizi nchini Afghanistan tangu mwanzoni mwa mwezi Mei, wakati Marekani na washirika wake NATO walipoanza kuondoa wanajeshi waliobaki kutoka nchini humo. Mashambulizi ya karibuni ya Taliban yaliliruhusu kundi hili kupata mafanikio katika maeneo mbali wakipata ushindi katika kipindi kidogo tu cha zaidi ya wiki moja, na kuishia kuanguka kwa serikali ya Afghanistan.

XS
SM
MD
LG