Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:24

Afghanistan : Muhtasari juu ya Taliban na historia yao


Kutoka Kushoto : Mkuu wa Baraza la Juu la Taifa la Maridhiano Abdullah Abdullah, Mwakilishi wa Qatar katika mapambano dhidi ya ugaidi Mutlaq al-Qahtani,
na kiongozi wa timu ya mazungumzo ya amani ya Taliban, Mullah Abdul Ghani Baradar (Photo by KARIM JAAFAR / AFP)
Kutoka Kushoto : Mkuu wa Baraza la Juu la Taifa la Maridhiano Abdullah Abdullah, Mwakilishi wa Qatar katika mapambano dhidi ya ugaidi Mutlaq al-Qahtani, na kiongozi wa timu ya mazungumzo ya amani ya Taliban, Mullah Abdul Ghani Baradar (Photo by KARIM JAAFAR / AFP)

Wapiganaji wa Taliban awali waliitawala Afghanistan kuanzia mwaka 1996 hadi 2001 na kuweka sheria kali za Kiislam nchini humo. Hizi ni baadhi ya taarifa sahihi juu ya Imani na historia ya kikundi hiki. 

Rais wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai (kushoto) na Muasisi mwenza wa Taliban Mullah Abdul Ghani Baradar (2R) wakihudhuria mkutano wa kimataifa juu ya Afghanistan kutafuta suluhisho la amani kutatua mgogoro wa Afghanistan huko Moscow Machi 18, 2021. (Photo by Alexander...
Rais wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai (kushoto) na Muasisi mwenza wa Taliban Mullah Abdul Ghani Baradar (2R) wakihudhuria mkutano wa kimataifa juu ya Afghanistan kutafuta suluhisho la amani kutatua mgogoro wa Afghanistan huko Moscow Machi 18, 2021. (Photo by Alexander...

Taliban iliundwa vipi?

Taliban ilikuwa ni mojawapo ya vikundi vinavyopigana vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Afghanistan katika miaka ya 1990 baada ya iliyokuwa Umoja wa Soviet kujiondoa nchini humo. Kikundi hicho kiliibuka tena mwaka 1994 katika eneo la kusini mwa Afghanistan katika mji wa Kandahar. Muasisi wao alikuwa Mullah Mohammad Omar, Imam katika msikiti wa mjini humo, ambaye aliwaongoza wanamgambo hao mpaka alipofariki mwaka 2013.

Nini mahusiano yao na Marekani?

Taliban awali ilikuwa na wanachama kutoka kilichokuwa kikundi cha wapiganaji wa Afghanistan, maarufu mujahedeen, ambao walikuwa wakisaidiwa na Marekani wakati wakipigana na iliyokuwa Umoja wa Soviet katika miaka ya 1980.

Kwa namna gani Taliban walichukua mamlaka?

Kufuatia kuondoka kwa Umoja wa Soviet kutoka Afghanistan mwaka 1989 na hatimaye kuanguka kwa serikali ya Afghanistan, nchi hiyo ilitumbukia katika vita vya wenyewe kawa wenyewe. Taliban walipata msaada wakiahidi kurejesha utulivu na haki. Mwaka 1994, walichukua udhibiti wa mji wa Kandahar bila ya upinzani mkubwa, na ilipofika mwaka 1996, walikuwa wameuteka mji mkuu, Kabul.

Taliban wana amini nini?

Taliban walitawala kwa kufuata tafsiri kali ya sheria za Kiislam. Mauaji ya hadharani na watu kupigwa viboko yalikuwa mambo ya kawaida, wanawake kwa kiwango kikubwa walikuwa walizuiliwa kufanya kazi au kusoma na walilazimishwa kuvaa nguo zinazowafunika mwili mzima, burqa katika maeneo ya umma. Taliban walipiga marufuku vitabu vya nchi za Magharibi na filamu na kuharibu vitu vya utamaduni vya tamaduni nyingine, ikiwemo masanamu makubwa yenye umri wa miaka 1,500 ya dhehebu la Buddha katika bonde la kati la Bamiyan.

Eneo la masanamu ya Buddha huko Bamiyan.
Eneo la masanamu ya Buddha huko Bamiyan.

Wana uhusiano gani na al-Qaida?

Taliban walitoa hifadhi kwa kundi la wanamgambo wa al-Qaida, lililokuwa wakati huo linaongozwa na Osama bin Laden. Al-Qaida iliweka kambi za mafunzo nchini Afghanistan, ambako lilikuwa likiandaa mashambulizi ya kigaidi kote duniani, ikiwemo shambulizi la Septemba 11, 2001 nchini Marekani.

Walipoteza vipi madaraka?

Chini ya mwezi mmoja baada ya mashambulizi ya Septemba 11, Marekani na washirika wake waliivamia Afghanistan. Mapema Disemba, serikali ya Taliban ilianguka, na Marekani ilianza kufanya kazi na raia wa Afghanistan kuunda serikali ya kidemokrasia.

Nini kilichofuata?

Kufuatia kushindwa kwao, viongozi wa Taliban walikimbilia kwenye ngome zao kusini na mashariki mwa Afghanistan au upande mwingine wa mpaka nchini Pakistan. Kundi la wanamgambo baadae liliongoza uasi dhidi ya serikali mpya ya Afghanistan iliyokuwa ikiungwa mkono na Marekani, wakitumia mabomu waliyotengeneza wenyewe na mashambulizi ya kujitoa muhanga.

Mwaka jana, serikali ya Marekani ilifanya mazungumzo kufikia makubaliano na Taliban baada ya zaidi ya miongo miwili ya kuhusika kijeshi nchini Afghanistan. Makubaliano hayo yaliweka ratiba kwa wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini humo kwa maelewano ya kuacha kuwashambulia Wamarekani na kuingia katika mazungumzo na serikali ya Afghanistan. Lakini, miezi ya mazungumzo kati ya Taliban na serikali ya Afghanistan yalishindwa kufanikisha makubaliano yoyote ya amani.

Nchi gani zimeitambua Taliban?

Ni nchi chache tu ziliitambua serikali ya Taliban wakati ilipokuwa inatawala kuanzia mwaka 1996-2001, ikiwemo Pakistan, Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken

Haiko wazi iwapo nchi nyingi zitaitambua serikali mpya ya Taliban; hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema mwezi uliopita kuwa Afghanistan itakuja kuwa serikali ya kidini kama Taliban itachukua madaraka kwa nguvu na kutenda ukatili.

XS
SM
MD
LG