Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:20

Moto wazuka uwanja wa ndege Kabul, afisa usalama wa Afghanistan auawa


Majeshi ya Marekani yakiimarisha ulinzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai, Kabul, Afghanistan, Agosti 20, 2021. Senior Airman Taylor Crul/U.S. Air Force/Handout
Majeshi ya Marekani yakiimarisha ulinzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai, Kabul, Afghanistan, Agosti 20, 2021. Senior Airman Taylor Crul/U.S. Air Force/Handout

Jeshi la Ujerumani limeripoti Jumatatu kuwa moto ulizuka nje ya lango la kaskazini katika uwanja wa ndege wa Kabul, huku washambuliaji wasiojulikana wakimuua afisa usalama wa Afghanistan na kuwajeruhi watatu wengine.

Jeshi la Ujerumani lilisema vikosi vyake na vile vya kutoka Marekani walihusika katika mapambano hayo.

Uwanja wa ndege umekuwa mahali pa kuhamishwa kwa umati wa watu unaofanywa na mataifa ya magharibi, hasa tangu Taliban ilipokamata mji mkuu wa Afghanistan, wiki moja iliyopita.

Maelfu ya raia wa Afghanistan wamefurika katika uwanja wa ndege wa Kabul kwa matumaini ya kupata nafasi kwenye moja ya ndege za kuwaondoa nchini humo.

Raia hao wanahofia kurudi kwa utawala wa tafsiri kali ya sharia za Kiislam, wakati Taliban ilipodhibiti nchi hiyo miaka 20 iliyopita.

Marekani imeshindwa kuwahamisha watu 5,000 hadi 9,000 kwa siku, na matukio ya machafuko Dani na karibu na uwanja wa ndege yamesababisha kukosolewa kwa juhudi zake hizo.

XS
SM
MD
LG