Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:11

Msafara wa kijeshi washambuliwa mashariki mwa DRC


Wanajeshi wa Congo washika doria kwenye jimbo la Kivu kaskazini kwenye picha ya awali
Wanajeshi wa Congo washika doria kwenye jimbo la Kivu kaskazini kwenye picha ya awali

Raia wanne wameuwawa huku darzeni kadhaa wakitekwa nyara Jumatano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya watu wansoshukiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu kuvamia msafara wa magari ya kijeshi na kuyachoma moto.  

Serikali imesema Jumatano kwamba tayari wanajeshi wake wameokoa zaidi ya watu 50 miongoni mwa waliotekwa nyara kwenye jimbo la Ituri na kwamba operesheni za kuokoa wenzao waliobaki zinaendelea. Kundi la Allied Democratic Forces, ama ADF, lenye mizizi yake nchini Uganda linashukiwa kutekeleza shambulizi hilo kulingana na wizara ya mawasiliano ya Congo.

Hata hivyo wizara hiyo haijasema ni watu wangapi waliotekwa nyara ingawa mbunge mmoja kutoka jimbo hilo awali alisema kwamba walikuwa takriban watu 80. Msafara ulioshambuliwa unasemekana kuwa wa takriban magari 100 yaliokuwa yakilindwa na jeshi wakati yakisafirisha watu na bidhaa kati ya miji ya Beni na Butembo.

Mashambulizi kutoka kwa makundi yenye silaha mashariki mwa Congo kwenye mpaka na Rwanda na Uganda yamekuwa yakiendelea licha ya serikali kuweka utawala wa kijeshi kwenye majimbo ya Ituri na Kivu kaskazini mwanzoni mwa mwezi Mei.

Watu walionusuria kwenye mashambulizi ya Jumatano wameambia shirika la habari la Reuters, kwamba risasi zilirushwa kutoka kila pande wakati baadhi ya magari yakiteketezwa muda mfupi baadaye.

XS
SM
MD
LG