Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:14

Polisi watumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji DRC


Martin Fayulu
Martin Fayulu

Polisi wa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Kinshasa wametawanya maandamano ya upinzani yaliyopigwa marufuku na maafisa wa usalama Jumatano ambapo polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na kuwakamata viongozi wa upinzani. 

Kulingana na shirika la habari la AFP watu wanane wamekamatwa akiwemo kiongozi wa upinzani Martin Fayulu aliyekuwa mgombania kiti cha rais wa muungano wa Lamuka wakati wa uchaguzi uliyopita.

Kiongozi wa kundi la kizazi kipya kwa ajili ya maendeleo ya Kongo Constant Mutamba anasema maandamano hayo yaliyoitishwa na lamuka yalikuwa na lengo la kupinga kuhusisha siasa kwenye Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, CENI, na kwamba muungano wa vyama vilivyo madarakani unataka kulazimisha mpango wake wa kuteua wajumbe wa tume hiyo ili kuwawezesha kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani.

"Sisi tumejitokeza ili kusisitiza kwamba hatutaki masuala ya kisiasa yahusishwe na tume ya CENI na kuwepo na maridhiano kuhusiana na mageuzi ya mfumo wa uchaguzi. Tunadhani muungano wa Union Sacree unaoshikilia madaraka hivi sasa unataka kulazimisha utekelezaji wa mpango wake ili kunyakua ushindi katika uchaguzi wa 2023," ameeleza Mutamba.

Mwanasiasa mwengine wa upinzani Adolphe Muzito ameliambia pia shirika la habari la AFP kwamba walipoanza maandamano katika mtaa wa Ndjili polisi na wanamgambio wao walijotokeza kwa wingi na kuwatawanya kwa kutumia gesi ya kutoa machozi

Inasikitisha kuoana waliyoko madarakani hivi sasa ni watu wale wale waliopigania kwa miaka mingi kuwepo kwa utawala wa sheria, wanafanya mambo haya. Inasikitisha pia kukandamizwa kwa namna hii na Tshisekedi na marafiki zake, Adolphe Muzito.

Muzito anasema wataitisha maandamano mengine hivi karibuni ili tuweze kuishinikiza serikali kwamba hawataki tume ya CENI inayoshawishiwa na wanasiasa wanataka tume huru isiyoingiliwa kati na upande wowote.

Maandamano kama hayo yaliitishwa kufanyika katika majimbo mengine ya Congo na katika mji wa kusini wa Lumbumbashi waandamanaji wanasemekana walitawanywa pia na polisi waliotumia mabomu ya kutoa machozi.

Rais Felix Tshisekedi mwanasiasa wa upinzani hapo zamani alichukua madaraka Januari 2019 kutoka kwa Joseph Kabila akiahidi uhuru wa kujieleza na kulinda haki za Binadam.

Uchaguzi ujao wa rais umepangwa kufanyika 2023 lakini utaratibu wa kuwateuwa wajumbe wa tume huru umekwama hivi sasa kwa muda wa wiki kadhaa ambapo upinzani wanapinga utaratibu uanaotaka kutumiwa na mungano uliyoko madarakani.

XS
SM
MD
LG