Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:40

Madaktari 20 wa DRC wamekufa kwa Corona tangu janga la Covid 19 lilipoingia nchini humo


Wauguzi wa afya huko DRC 2020 walipoandamana kudai mishahara (VOA/Charly Kasereka)
Wauguzi wa afya huko DRC 2020 walipoandamana kudai mishahara (VOA/Charly Kasereka)

Tayari tumepoteza  madaktari 20 ambao wamekufa kwa ugonjwa wa virusi vya Corona katika mkoa wa Kivu Kusini tangu kutangazwa kwa janga hilo hapo Machi mwaka 2020 aliliambia shirika la habari la AFP Dr. Muhunjuka Bajambaka rais wa umoja wa madaktari wa Kivu Kusini

Madaktari 20 wa Congo wamekufa baada ya kupata maambukizi ya virusi vya Corona katika zaidi ya kesi 1,500 zilizorekodiwa tangu mwezi Machi mwaka 2020 katika jimbo la Kivu Kusini huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DCR).

Tayari tumepoteza madaktari 20 ambao wamekufa kwa ugonjwa wa virusi vya Corona katika mkoa wa Kivu Kusini tangu kutangazwa kwa janga hilo hapo Machi mwaka 2020 aliliambia shirika la habari la AFP Dr. Muhunjuka Bajambaka rais wa umoja wa madaktari wa Kivu Kusini. Hali hii inatokana na ukweli kwamba hali ya mazingira ya kufanyia kazi hayakidhi na wauguzi wanaambukizwa, aliongeza.

DRC imekuwa ikipambana na wimbi la tatu la maambukizi tangu Mei. Nchi hiyo imerekodi kesi 49,562 za COVID-19 na vifo 1,023 pamoja na watu 29,497 waliotangazwa kupona kulingana na ripoti rasmi ya hivi karibuni iliyochapiswa Ijumaa.

Pamoja na kesi 1,571 Kivu Kusini inashika nafasi ya tano kwa idadi ya maambukizi wakati jimbo jirani la Kivu Kaskazini lina jumla ya kesi 4,632. Shughuli nyingi za watu zinaripotiwa kila siku kati ya majimbo hayo mawili.

XS
SM
MD
LG