Shambulizi hilo limetokea katika njia kuu kati ya miji ya Maimoya na Chani-chani, kiasi cha kilomita 40 kutoka mji wa Beni, jimbo la Kivu Kaskazini.
Lori hilo lilikuwa likitoka sokoni Pa Chanichani magharibi mwa Maimoya wilayani Beni kutoka Oicha , wengi wa waathirika wa mauaji hayo ni wanawake ambao walikuwa wakitoka sokoni kununua chakula.
Jeshi la Congo FARDC limefika eneo la tukio kutafuta mili ya watu iliyokuwa imefichwa porini na vile vile pikipiki zilizo shambuliwa na kuchomwa na waasi. Mili yote ilipelekewa Oicha Beni ili kusubiri matayarisho ya mazishi.
Shambulizi hili linakuja wakati ambapo Mkoa wa Kivu kaskazini unaongozwa na Gavana wa kijeshi ambaye yuko Beni.
Wananchi wanaelezea tukio hilo kuwa baya na kupoteza matumaini kwa hatua ya Rais Felix Tshisekedi aliyochukuwa kuweka viongozi wa kijeshi kumaliza uasi katika eneo hilo ambako watu zaidi ya elfu sita wameshapoteza maisha tangu 2013 hadi sasa