Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:00

DRC : Wananachi wenye hasira wachoma moto ukumbi wa ofisi za jiji Beni


Beni, DRC
Beni, DRC

Wananchi wenye hamasa mapema Jumatatu wamewasha moto ukumbi wa jiji kwenye mji wenye ghasia wa Beni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Hili ni kufuatia mauaji ya watu 8 yaliyofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa kundi la waasi la ADF.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, msemaji wa jeshi la DRC kanali Mak Hazukai amethibitisha mauaji hayo yalitokea karibu na mpaka wa DRC na Uganda.

Kamanda huyo amesema washambuliaji waliingia kwenye ukumbi wa Boikena na kuuwa raia hao.

Baada ya kuwasha moto huo, mwandishi wa AFP alieshuhudia amesema kuwa watu waliandamana wakielekea kwenye kambi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa MUNUSCO ilioko nje kidogo ya Beni.

Kumekuwa na maandamano katika siku za karibuni dhidi ya walinda amani mjini Beni wanaolaumiwa kushindwa kuzuia mashambulizi ya mara kwa mara yanayo daiwa kufanywa na kundi la wapiganaji la Allied Democratic Forces, ADF.

Karibu watu 70 wameuawa mjini Beni tangu operesheni ya kijeshi dhidi ADF ilipoanza Novemba mwaka 2018.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG