Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:32

Wananchi wa DRC watofautiana juu ya Ntaganda kufungwa miaka 30


Bosco Ntaganda
Bosco Ntaganda

Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wametoa maoni yanayo hitalafiana Alhamisi kufuatia hukumu ya kifungo cha miaka 30 alichopewa kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo waasi la UPC, Bosco Ntaganda, na mahakama ya uhalifu wa kimataifa, ICC, mjini The Hague.

Baadhi ya wananchi wa mashariki ya DRC wanasema hukumu hiyo ni muda mchache huku watu wakabila lake wakidai kwamba ni uwonevu kwani kuna viongozi wengine wa Kongo wanaostahiki kupelekwa pia mbele ya ICC.

Mahakimu wa mahakama ya ICC Alhamisi walitoa hukumu Ntaganda atumikie kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya mauaji, ubakaji na kuwalazimisha watoto kujiunga na wapiganaji wa kundi lake la waasi.

Ntaganda mwenye umri wa miaka 46 alikutwa na hatia ya makosa 18 ya uhalifu wa kivita na uahalifu dhidi ya ubinadamu kwa ushiriki wake wakati wa operesheni za kijeshi mashariki mwa DRC, mwaka 2002 hadi 2003.

Ntaganda aliyekuwa amevalia suti ya rangi nyeusi alionekana kusikiliza kwa makini uamuzi wa jaji. Imeelezwa kuwa tayari alishakata rufaa kuhusu kukamatwa kwake.

Wakati wa ghasia huko DRC, Ntganda na jopo lake la wanajeshi wa UPC wengi kutoka kabila la Hema waliwalenga kabila la Lendu kwenye jimbo lenye utajiri wa madini la Ituri.

Mamia ya raia waliuwawa na wengine kulazimika kutorokea maeneo mengine.

Katika hukumu hiyo Jaji Robert Fremr alisema ntagandwa sio tu anawajibishwa kwa uhali wa binadamu bali binafsi alimuuwa kasisi wa kanisa katoliki na kuweka mfano kwa wafuasi wake kufuata.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG