Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:45

ICC yasema Bemba aachiwe huru


Jean Pierre Bemba akiwa mahakamani, tjhe Hague June 8, 2018. (Twitter/CPI)
Jean Pierre Bemba akiwa mahakamani, tjhe Hague June 8, 2018. (Twitter/CPI)

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu – ICC - imeamua kwamba makamu wa rais wa zamani wa DRC, Jean Pierre Bemba, atolewe gerezani mara moja, kufuatia hatua ya wiki iliyopita iliyomwondolea hatia ya mashitaka ya uhalifu wa wakati wa vita aliyokutwa nayo na hatia miaka kadha iliyopita. Bemba bado anakabiliwa na hatia katika mashitaka tofauti ya kuingilia kati ushahidi.

Wachambuzi wanasema kuachiwa kwake huenda kukawa na athari kubwa katika uchaguzi wa DRC.

Bemba anakabiliwa na hadi miaka mitano jela katika mashitika ya kuingilia kati ushahidi, shitaka ambalo alishindwa katika mahakama ya rufaa.

Lakini alipata ushindi mkubwa wiki iliyopita katika kesi kubwa dhidi yake ya uhalifu wa kivita. Mahakama ya rufaa ya ICC ilitengua hatia dhidi yake kwa mauaji yaliyofanywa na kundi lake la MLC katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati katika miaka ya mwanzoni ya 2000.

Katika uamuzi wa majaji 3-2 mahakama ilisema Bemba hawezi kuwajibishwa kwa vitendo vya majeshi ya MLC, vingine ambavyo vilitokea wakati Bemba ni makamu wa rais wa DRC.

Mwanasheria wake Melinda Taylor alisema anastahili kuachiwa kutoka gerezani mara moja wakati anasubiri adhabu katika kesi ya kuingilia kati ushahidi. Hata hivyo, mawakili wa upande wa mashitaka wanasema kukutwa kwake na hatia katika kesi hiyo ina maana huenda asitolewe karibuni.

Mwanasheria wake anasema Bemba anataka kujiunga na familia yake Ubelgiji, lakini swala lake la kisheria huenda pia likaathiri uchaguzi wa DRC unaotazamiwa baadaye mwaka huu.

XS
SM
MD
LG