Shambulizi la Alhamisi ni mwendelezo wa mauaji yanayoripotiwa kutekelezwa na makundi ya waasi nchini Congo.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, UN, Kundi la waasi la ADF kutoka Uganda, linalofanya mashambulizi ya kila mara mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa zaidi ya miongo mitatu, hadi sasa limeua zaidi ya watu 1,000 tangu mwaka 2019.
UN umehusisha mashambulizi hayo ambayo yameongezeka kwa kiasi kikubwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, na kaunzishwa kwa msako wa jeshi la taifa dhidi ya makundi ya waasi.