Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:02

Kamerhe akutwa na hatia, afungwa miaka 20


Vital Kamerhe, kushoto, akiwa na Felix Tshisekedi mjini Nairobi wakati wa kuelekea uchaguzi wa DRC, 2018
Vital Kamerhe, kushoto, akiwa na Felix Tshisekedi mjini Nairobi wakati wa kuelekea uchaguzi wa DRC, 2018

Mahakama mjini Kinshasa nchini DRC imemhukumu miaka 20 jela Vital Kamerhe aliyekuwa mkuu wa utawala katika Ofisi ya Rais Felix Tshisekedi baada ya kumkuta na hatia katika mashitaka ya wizi wa pesa na matumizi mabaya ya fedha za serikali katika miradi ya maendeleo ya siku mia moja .

Kamerhe aliyewahi kuwa spika wa bunge la taifa katika utawala wa Rais Joseph Kabila ni mmoja wa watu wa karibu sana na Rais Tshisekedi na ndie aliye msaidia wakati wa kampeni ya uchaguzi hadi kuingia madarakani.

Vital Kamerhe amesema mashitaka hayo yalikuwa ya kisiasa na atakata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Mara baada ya hukumu hiyo kutangazwa milio ya risasi imesikika katika mji wa Buka Kivu kusini mwa nchi ambako ni nyumbani kwa Kamerhe na wafuasi wa chama chake cha UNC wamesema hawatakubali kiongozi wao kuwekwa gerezani wakidai kuwa kesi dhidi ya kiongozi wao ni ya kisiasa.

Polisi na jeshi wamezuia waandamanaji walio jaribu kuandamana na kuvuruga shughuli za kibiashara.

Polisi wametawanywa pia sehemu mbali mbali katika miji ya Goma na Bukavu kulinda usalama endapo kutatokea vurugu.

Imeripotiwa na Austere Malivika, Sauti ya Amerika, Goma.

XS
SM
MD
LG