Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:45

UN yaanza kumlinda mshindi wa Nobel, Denis Mukwege, DRC


Dr Denis Mukwege, mshindi wa Nobeli 2018 akiwa na walinda amani.
Dr Denis Mukwege, mshindi wa Nobeli 2018 akiwa na walinda amani.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa, Jumatano wameanza kumlinda mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Denis Mukwege wa jamhuri ya kidemokrasia ya congo - DRC, ambaye ametishiwa kuuwawa katika wiki za hivi karibuni, baada ya kutaka kupatikana haki katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo.

Mukwege ameshinda tuzo mbalimbali za kimataifa, ikiwemo ile ya Nobel ya mwaka 2018, kwa kufanyakazi kwa miongo kadhaa kutibu wanawake walioathirika na mgogoro wa kisiasa mjini Bukavu, DRC.

Kwa kipindi kirefu ameshiriki katika katika mahakama za kimataifa za kusikiliza mashitaka ya uhalifu wa kivita yaliyofanyika kati ya mwaka 1993 na 2003, pamoja na hukumu za makundi ya wenye silaha yaliyohusika kwa matendo ya udhalilishaji wa kingono mashariki mwa DRC.

Maoni ya hivi karibuni ya Mukwege, yamemfanya aingie katika mgogoro na taifa jirani la Rwanda, ambalo waziri wake wa ulinzi mwezi uliopita alimshutumu Mukwege kwa kusambaza propaganda.

Umoja wa Mataifa ulisimamisha ulinzi wake mwezi Mei, kwa sababu ya janga la virusi vya Corona, baada ya walinda amani ambao walikuwa wamepangiwa kulinda hospitali ya Panzi kupata maambukizi.

Mathias Gillmann, msemaji wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, alisema kwamba walinda amani wamerejea kuhakikisha hospitali ya Panzi inakuwa na ulinzi.

Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kuwafundisha mapolisi wa eneo hilo kwa ajili ya kufanya ulinzi kwa kipindi kirefu zaidi.

Wiki iliyopita, maelfu ya watu wanaomuunga mkono Mukwege, waliandamana katika mitaa ya Bukavu wakitaka apatiwe ulinzi.

XS
SM
MD
LG