Maafisa wa usalama wanamtafuta mwanajeshi huyo katika mji wa Sange, kilomita 24 kutoka mpaka wa Burundi ambapo tukio hilo lilitokea alhamisi jioni.
Taarifa kutoka kwa ofisi ya gavana wa jimbo la Kivu Kusini, Theo Kasi, imethibitisha tukio hilo.
Idadi kubwa ya wanajeshi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wanaripotiwa kutopata mafunzo mazuri na ya kutosha.
Wanajeshi hao wameshutumiwa mara nyingi kwa vitendo vya uhalifu dhidi ya raia.
Marekani na umoja wa ulaya zimewawekea vikwazo majenerali kadhaa kwa madai ya kutoa silaha kwa makundi ya wapiganaji na wahalifu nchini humo.
Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC.