Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:12

UNHCR yatoa wito wanawake na wasichana walindwe dhidi ya mashambulizi ya ngono DRC


Wanawake wa Congo na watoto akiwasili katika kituo cha mpakani huko Chissanda, katika mkoani wa Lunda Norte, baada ya kukimbia mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo katika mkoa wa Kasai, DRC, May 2017. © UNHCR / Pumla Rulashe
Wanawake wa Congo na watoto akiwasili katika kituo cha mpakani huko Chissanda, katika mkoani wa Lunda Norte, baada ya kukimbia mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo katika mkoa wa Kasai, DRC, May 2017. © UNHCR / Pumla Rulashe

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, linaitaka serikali ya Congo kuongeza usalama na kuwalinda wanawake na wasichana kutokana na kusambaa kwa mashambulizi ya ngono yanayofanywa na makundi hasimu yenye silaha katika jimbo la Tanganyika nchini DRC.

Mashambulizi ya kutisha sana dhidi ya wanawake na wasichana yanafanyika katika eneo ambalo linaitwa “triangle of death”. Eneo hili linapakana na maeneo kadhaa Jirani kati ya majimbo ya Tanganyika, Maniema na Kivu Kusini.

Katika muda wa wiki mbili zilizopita, mashirika ya misaada yamerekodi matukio 243 ya ubakaji, ikiwemo ubakaji waliofanyiwa watoto 48. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linasema takwimu hizi zinatisha san ana ni za juu mno, lakini hazionyeshi kiwango cha kweli na ukubwa wa uhalifu huu.

Msemaji wa UNHCR Shabia Mantoo anasema idadi ya kweli inadhaniwa kuwa kubwa zaidi. Anasema katika kesi nyingi manyanyaso ya ngono hayariopotiwi. Hii ni kwasababu ya manyanyaso ya kijinsia bado kwa kiasi kikubwa ni mwiko kuyazungumzia na wanawake ambao wanakumbwa na manyanyaso haya wanaweza kukabiliwa na unyanyapaa na kutengwa na familia zao.

Benta Loma mwenye umri wa miaka 20 alikamatwa alishiriki katika maandamano Kinshasa akilaani vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake katika mkoa wa Kasai, DRC.(C. Oduah/VOA
Benta Loma mwenye umri wa miaka 20 alikamatwa alishiriki katika maandamano Kinshasa akilaani vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake katika mkoa wa Kasai, DRC.(C. Oduah/VOA

Mantoo amesema “Mashambulizi yanaripotiwa kuwa yalifanywa na makundi hasimu yenye silaha wakishindania udhibiti wa maeneo ya madini, hasa machimbo ya dhahabu – ikiwa kama hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya operesheni zinazoongozwa na jeshi la serikali. Raia wamejikuta wamekwama katikati ya mapambano makali sana kati ya makundi tofauti.”

Ghasia na ukosefu wa usalama katika eneo hili umesababisha takriban watu 310,000 kukimbia makazi yao. Maafisa wa kieneo wameripoti zaidi ya watu elfu 23 wamekoseshwa makazi tangu mwezi May huko kaskazini mwa Tanganyika katika eneo la Kongolo pekee. Wanasema wengi wamekimbia ukosefu wa usalama mara kadhaa katika muda wa miezi mitatu iliyopita.

Mantoo anasema wastani wa mashambulizi 17 ya ngono yaliripotiwa kila siku. anasema waathirika wa ubakaji wanakumbwa na matatizo makubwa ya kimwili na kiwewe cha kisaikolohia lakini wanapta taabu kupata msaada wa afya na huduma za kisaikolojia wanaohitaji.

“Wafanyakazi wetu wamesikia ushuhuda wa kutisha sana wa ghasia zilizokithiri. Watu wakikoseshwa makazi kwa nguvu na kuyashutumu makundi yenye silaha ambayo yamefanywa ubakaji wa watu wengi hasa wanawake ambao walijaribu kukimbia makwao. Baadhi ya wanawake na wasichana wametekwa na kutumia kama watumwa wa ngono na wanachama wa makundi yenye silaha. Familia zimetakiwa kulipa fidia kwa mabadilishano ya uhuru wa jamaa zao,” amesema Mantoo.

UNHCR inaisihi serikali ya Congo kufanya mengi zaidi kuwalinda raia, hasa wanawake na wasichana, na kuhakikisha kuwa fursa ya misaada ya kibinadamu inawafikia wale wasiokuwa na makazi. Pia inataka uchunguzi ufanyike kuhusu ukatili uliotendwa na kwa watenda maovu kufikishwa mbele ya sheria.

UNCHR inaomba msaada zaidi ya kimataifa, ikisema kuwa imepata asilimai 36 tu ya takriban dola milioni 205 ambao zinahitajika kwa ajili ya operesheni za nchin DRC.

XS
SM
MD
LG