Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 20:43

DRC yakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizo ya corona


Dr. Jean-Jacques Muyembe mkuu wa sekretariat ya kupambana na covid-19 akiwa na rais président Félix Tshisekedi katika ikulu ya Kinshasa, Februari 11,. 2021. (Twitter/Présidence RDC)
Dr. Jean-Jacques Muyembe mkuu wa sekretariat ya kupambana na covid-19 akiwa na rais président Félix Tshisekedi katika ikulu ya Kinshasa, Februari 11,. 2021. (Twitter/Présidence RDC)

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizo ya corona, na huku kitovu kikiwa katika mji mkuu, Kinshasa, ikiwa ni moja ya miji yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, Waziri wa Afya Jean-Jacques Mbungani alisema Alhamisi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kama nchi nyingine nyingi za Kiafrika, Congo imeripoti visa na vifo vichache, lakini maafisa wa afya wana wasiwasi juu ya kuongezeka kwa hivi karibuni kwa maambukizo ambayo yalisababisha visa vipya 243 vilivyorekodiwa Jumatano, idadi kubwa zaidi ya kila siku tangu mwezi Machi.

“Natangaza rasmi kuanza kwa wimbi la tatu la janga la COVID-19 katika nchi yetu, Kinshasa ikiwa kitovu chake”, Mbungani aliwaambia waandishi wa habari.

Kiwango cha chini cha chanjo na kutozingatia kanuni za usafi zilizopendekezwa zilikuwa ni sababu za kuongezeka kwa kiwango cha maambukizo, alisema.

XS
SM
MD
LG