Watu wenye silaha waliokua kwenye pikipiki mwezi uliopita walimshambulia kwa bunduki, waziri wa kazi na uchukuzi na mkuu wa zamani wa polisi, Katumba Wamala, alipokuwa ndani ya gari lake akiwa kwenye kitongoji kimoja cha Kampala.
Washukiwa ni sehemu ya kundi lililopewa mafunzo katika kambi moja kwenye jimbo la Kivu kaskazini, kambi inayoendeshwa na kundi la waasi wa Allied Democratic Forces,ADF, naibu mkuu wa polisi Paul Lokech amesema. ADF linadai kutokuwa na uhusiano na kundi la Islamic State.
Kundi hilo awali lilianzishwa nchini Uganda, lakini kwa sasa linaendesha operesheni zake katika misitu mashariki mwa DRC. Jumatatu, washukiwa wawili walishtakiwa kwa kuhusika kwao katika shambulizi hilo, lakini maafisa wa usalama hawakutoa maelezo zaidi ya uchunguzi wao