Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:03

SADC yaisifu Zambia kwa makabidhiano ya madaraka ya amani


Rais mteule wa Zambia Hakainde Hichilema akizungumza na waandishi wa habari.
Rais mteule wa Zambia Hakainde Hichilema akizungumza na waandishi wa habari.

Ni mara ya tatu kwa  kubadilishana madaraka kwa amani  na upinzani nchini Zambia tangu 1991

Ni mara ya tatu kwa kubadilishana madaraka kwa amani na upinzani nchini Zambia tangu 1991, katika bara ambalo viongozi waliopo madarakani mara nyingi wanashikilia madaraka kwa miongo kadhaa.

Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, akifungua mkutano wa viongozi wa kusini mwa Afrika-SADC mjini Lilongwe hivi alisema mwenendo wa makabidhiano ya madaraka kwa amani ambayo tumeshuhudia katika eneo letu katika miaka ya hivi karibuni, huku Zambia ikiwa mwanachama wa hivi karibuni kufanya hiyo wanastahili sifa kimataifa.

Mkutano wa viongozi mjini Lilongwe utaangalia maendeleo yaliyopatikana katika kukuza na kuongeza ushirikiano wa kikanda kulingana na Dira ya 2050 ya SADC, ambayo inafikiria kuleta nchi zenye kipato cha kati mpaka juu zenye viwanda ambapo raia wote watafurahia ustawi endelevu wa uchumi, haki , na uhuru.

Katibu mtendaji wa SADC Stergomena Lawrence Tax ataondoka baada ya kuhudumu kwa miaka nane, na katibu mtendaji mpya ataapishwa.

Botswana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zote zimeteua wagombea wa nafasi hiyo.

Botswana inataka Elias Mpedi Magosi kuchukua nafasi hiyo wakati DRC imemtaja Faustin Luanga Mukela kama mgombea wake wa wadhifa huo wa juu wa SADC.

Wakati wa mkutano wa 41, Rais wa Malawi, Lazarus McCarthy Chakwera, atachukua uenyekiti wa SADC kutoka kwa Filipe Jacinto Nyusi, Rais wa Msumbiji.

XS
SM
MD
LG