Kampuni hiyo imeeleza inataka kunufaika na mahitaji yanayo ongezeka ya usafiri wa ndege barani Afrika.
Jambojet ambayo ilianzishwa mwaka 2014 na kumilikiwa na kampuni ya taifa ya Kenya Airways inataraji Afrika kuwa mojawapo ya kanda zitakazo kuwa na ukuaji wa haraka wa usafiri wa ndege duniani mnamo miongo miwili ijayo ambapo inakadiriwa itaongezeka kwa asili mia 5 kila mwaka.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo Vincent Rague akitangaza habari hizo amesema wanataka kuwa sehemu ya ukuaji huo.
Jambojet itasafiri hadi Goma mara mbili kwa wiki kutokea Nairobi kabla ya kuongeza safari zake hadi mara nne kwa wiki katika miezi ijayo.
Chanzo cha Habari hii ni Shirika la Habari la Reuters